Masharti ya matumizi
Masharti yaliyo wazi kwa booking salama.
Hapa tunaeleza booking, malipo, cancellation, refund na wajibu wa kila upande.
Jukumu la KODIMALI
KODIMALI huunganisha wateja na wamiliki, mameneja au mawakala waliothibitishwa, na kutoa zana za kutafuta, kufanya booking, kulipa na kufuatilia huduma. Isiposemwa wazi kwenye muamala, KODIMALI si mmiliki wa mali wala mhusika wa mkataba wa upangishaji.
Booking na malipo
Kwa listing inayoruhusu instant booking, mfumo hukagua muda uliochagua na kuushikilia kwa dakika 30. Hold si booking iliyolipwa; booking inathibitishwa baada ya malipo kukamilika. Hold huisha ikiwa malipo hayajakamilika kwa muda ulioonyeshwa.
Kiasi kamili, madhumuni ya malipo, muda na listing vitaonyeshwa kabla ya kuidhinisha ombi la mobile money. Mfumo huzuia booking mbili zinazogongana kwa muda mmoja. Viewing ni hiari na si sharti la kufanya booking.
Cancellation na refund
Uwezo wa kufanya cancellation na kiasi kinachoweza kurejeshwa hutegemea sera iliyoonyeshwa kwa booking husika, muda uliobaki kabla ya kuanza huduma, na kama huduma tayari imeanza. Ombi la refund hukaguliwa; si kila malipo hurudishwa moja kwa moja.
Refund iliyoidhinishwa hurudishwa kwa njia ya awali ya malipo inapowezekana. Muda wa kuonekana kwa fedha hutegemea mtoa huduma wa malipo. Hifadhi uthibitisho wa malipo na mawasiliano ya booking kwa ajili ya ukaguzi.
Kulipia mawasiliano
Malipo ya kufungua namba ya wakala ni ada ya kupata mawasiliano kwa muda ulioonyeshwa; si kodi, deposit wala booking. Ikiwa listing haipatikani au wakala hajibu, unaweza kuomba ukaguzi wa refund kupitia msaada wa KODIMALI.
Wajibu wa mmiliki au wakala
Wamiliki, mameneja na mawakala lazima waweke taarifa sahihi, ruhusa halali, bei na availability ya sasa. Booking iliyothibitishwa lazima iheshimiwe. Mabadiliko yanayoweza kuathiri mteja yawasilishwe haraka kupitia mfumo.
Matukio na quotation
Kwa mpango wa tukio wenye watoa huduma wengi, quotation na mbadala wowote huwasilishwa kwanza. Makubaliano, deposit au malipo huanza tu baada ya mteja kuona na kukubali maelezo husika.
Usalama na migogoro
KODIMALI inaweza kukagua, kuzuia au kuondoa akaunti, listing au muamala ili kulinda watumiaji. Ripoti tatizo kupitia msaada wa KODIMALI ukiambatanisha booking reference, uthibitisho wa malipo na maelezo muhimu.